1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2 Laiti uchungu wangu ungepimwa,Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!
3 Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari;Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
4 Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu,Na roho yangu inainywa sumu yake;Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.