5 Je! Huyo punda-mwitu hulia akiwa na majani?Au, ng’ombe hulia malishoni?
6 Je! Kitu kisicho na ladha yumkini kulika pasipo chumvi?Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?
7 Roho yangu inakataa hata kuvigusa;Kwangu mimi ni kama chakula kichukizacho.
8 Laiti ningepewa haja yangu,Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!
9 Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniseta;Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
10 Hapo ndipo ningefarijika hata sasa;Naam, ningejikuza katika maumivu yasiyoniacha;Kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.
11 Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje?Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?