Ayu.
Sura 7:12-18
Swahili Union Version
12Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi?Hata ukawaweka walinzi juu yangu?
13Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo,Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;
14Ndipo unitishapo kwa ndoto,Na kunitia hofu kwa maono;
15Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa,Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.
16 Ninadhoofika; sitaishi sikuzote;Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.
17 Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza,Na kumtia moyoni mwako,
18Na kumwangalia kila asubuhi,Na kumjaribu kila dakika?