9 Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
10 Hatarudi tena nyumbani kwake,Wala mahali pake hapatamjua tena.
11 Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu;Nitanena kwa mateso ya roho yangu;Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.
12 Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi?Hata ukawaweka walinzi juu yangu?
13 Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo,Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;
14 Ndipo unitishapo kwa ndoto,Na kunitia hofu kwa maono;
15 Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa,Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.