1 Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,
2 Wewe utanena maneno haya hata lini?Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini?
3 Je! Mungu hupotosha hukumu?Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?
4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;
5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,Na kumsihi huyo Mwenyezi;