1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 Kweli najua kuwa ndivyo hivyo;Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?
3 Kama akipenda kushindana naye,Hawezi kumjibu neno moja katika elfu.
4 Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu;Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?
5 Aiondoaye milima, nayo haina habari,Akiipindua katika hasira zake.
6 Aitikisaye dunia itoke mahali pake,Na nguzo zake hutetema.