11 Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone;Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue.
12 Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia?Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini?
13 Mungu haondoi hasira zake;Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
14 Je! Mimi nitamjibuje,Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye?
15 Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu;Ningemsihi-sihi mtesi wangu.
16 Kama ningemwita, naye akaniitikia;Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu.
17 Yeye anipondaye kwa dhoruba,Na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu.