20 Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu;Ingawa ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa ni mpotovu.
21 Mimi ni mkamilifu; siangalii nafsi yangu;Naudharau uhai wangu.
22 Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema,Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia.
23 Kama hilo pigo likiua ghafula,Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa.
24 Dunia imetiwa mkononi mwa waovu;Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake;Kama si yeye, ni nani basi?
25 Basi siku zangu zina mbio kuliko tarishi;Zakimbia, wala hazioni mema.
26 Zimepita kama merikebu ziendazo mbio;Mfano wa tai ayashukiaye mawindo.