27 Nikisema, Mimi nitasahau kuugua kwangu,Nitaacha kununa uso nikachangamke moyo;
28 Mimi huziogopa huzuni zangu zote,Najua kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
29 Nitahukumiwa kuwa ni mkosa;Ya nini basi nitaabike bure?
30 Ingawaje najiosha kwa maji ya theluji,Na kuitakasa mikono yangu kwa sabuni;
31 Lakini utanitupa shimoni,Nami hata nguo zangu zitanichukia.
32 Kwani yeye si mtu, kama mimi, hata nimjibu,Hata tukaribiane katika hukumu.
33 Hapana mwenye kuamua katikati yetu,Awezaye kutuwekea mkono sote wawili.