5 Aiondoaye milima, nayo haina habari,Akiipindua katika hasira zake.
6 Aitikisaye dunia itoke mahali pake,Na nguzo zake hutetema.
7 Aliamuruye jua, nalo halichomozi;Nazo nyota huzipiga muhuri.
8 Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu,Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9 Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia,Na makundi ya nyota ya kusini.
10 Atendaye mambo makuu yasiyotafutikana;Naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
11 Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone;Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue.