8 Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu.
9 Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.
10 Ewe niliyekufikicha, na nafaka ya sakafu yangu; Hayo niliyoyasikia kwa BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, nimewapasha habari zake.
11 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?
12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.
13 Ufunuo juu ya Arabuni.Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala,Enyi misafara ya Wadedani.
14 Waleteeni wenye kiu maji,Enyi wenyeji wa nchi ya Tema;Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.