1 Ufunuo juu ya bonde la maono.Sasa una nini, wewe,Hata umepanda pia juu ya dari za nyumba?
2 Ewe uliyejaa makelele,Mji wa ghasia, mji wenye furaha;Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga,Wala hawakufa vitani.
3 Wakuu wako wote wamekimbia pamoja,Wamefungwa wasiutumie upinde.Wote walioonekana wamefungwa pamoja,Wamekimbia mbali sana.
4 Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu.
5 Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.