2 Ewe uliyejaa makelele,Mji wa ghasia, mji wenye furaha;Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga,Wala hawakufa vitani.
3 Wakuu wako wote wamekimbia pamoja,Wamefungwa wasiutumie upinde.Wote walioonekana wamefungwa pamoja,Wamekimbia mbali sana.
4 Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu.
5 Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
6 Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao.
7 Hata ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga wakielekea malango.
8 Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda, nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni.