16 BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na BWANA ataifunua aibu yao.
18 Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;
19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;
20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;
21 na pete, na azama,
22 na mavazi ya sikukuu, na debwani; na shali, na vifuko;