16 Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana.
17 Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
18 Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.
19 Lakini mvua ya mawe itakunya, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.
20 Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng’ombe na punda waende ko kote.