14 Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia;Naliomboleza kama hua;macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu;Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
15 Niseme nini? Yeye amenena nami,na yeye mwenyewe ametenda hayo;Nitakwenda polepole miaka yangu yote,kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
16 Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi;Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote;Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.
17 Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu;Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu;Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
18 Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu;mauti haiwezi kukuadhimisha;Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.
19 Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo;Baba atawajulisha watoto kweli yako.
20 BWANA yu tayari kunipa wokovu.Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu,Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.