19 Mambo haya mawili yamekupata;Ni nani awezaye kukusikitikia?Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga;Niwezeje kukutuliza?
20 Wana wako wamezimia,Wamelala penye pembe za njia kuu zoteKama kulungu wavuni;Wamejaa hasira ya BWANA,Lawama ya Mungu wako.
21 Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo;
22 BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena;
23 nami nitakitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.