1 Ni nani huyu atokaye Edomu,Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra?Huyu aliye na nguo za fahari,Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?Mimi nisemaye kwa haki,Hodari wa kuokoa.
2 Kwani mavazi yako kuwa mekundu,Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?
3 Nalikanyaga shinikizoni peke yangu;Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu,Naliwaponda kwa ghadhabu yangu;Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao,Nami nimezichafua nguo zangu zote.
4 Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu,Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.
5 Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia;Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza;Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu,Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
6 Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu,Nikawalevya kwa ghadhabu yangu,Nami nikaimwaga damu yao chini.
7 Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.