10 Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.
11 Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu?
12 Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kuume wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele?
13 Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae?
14 Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
15 Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
16 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.