17 Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote.
18 Kama vile vilivyotokea wakati wa kuangushwa Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.
19 Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
20 Basi, lisikieni shauri la BWANA;Alilolifanya juu ya Edomu;Na makusudi yake aliyoyakusudiaJuu yao wakaao Temani;Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi;Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
21 Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao;Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu.
22 Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake.
23 Habari za Dameski.Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia;Maana wamesikia habari mbaya;Wameyeyuka kabisa;Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.