21 Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema BWANA, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia.
22 Pana mshindo wa vita katika nchi,Mshindo wa uharibifu mkuu.
23 Imekuwaje nyundo ya dunia yoteKukatiliwa mbali na kuvunjwa?Imekuwaje Babeli kuwa ukiwaKatikati ya mataifa?
24 Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.
25 BWANA amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo.
26 Njoni juu yake toka mpaka ulio mbali;Zifungueni ghala zake;Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa;Msimsazie kitu cho chote.
27 Wachinjeni mafahali wake wote;Na watelemkie machinjoni;Ole wao! Maana siku yao imewadia,Wakati wa kujiliwa kwao.