1 Maneno ya Amosi, mmojawapo wa wachungaji wa mji wa Tekoa. Mungu alimfunulia Amosi mambo haya yote kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya lile tetemeko la ardhi, wakati Uzia alipokuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yoashi, alipokuwa mfalme wa Israeli.
2 Amosi alisema hivi:Mwenyezi-Mungu ananguruma kutoka mlima Siyoni,anavumisha sauti yake kutoka Yerusalemu,hata malisho ya wachungaji yanakauka,nyasi mlimani Karmeli zinanyauka.
3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Damasko wametenda dhambi tena na tena;kwa hiyo, sitaacha kuwaadhibu;waliwatendea watu wa Gileadi ukatili mbaya.
4 Basi, nitaishushia moto ikulu ya mfalme Hazaeli,nao utaziteketeza kabisa ngome za mfalme Ben-hadadi.
5 Nitayavunjavunja malango ya mji wa Damasko,na kuwang'oa wakazi wa bonde la Aweni,pamoja na mtawala wa Beth-edeni.Watu wa Aramu watapelekwa uhamishoni Kiri.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
6 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka watu kabila zima,wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.