6 Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni,nayo dunia akaifunika kwa anga;huyaita maji ya bahari,na kuyamwaga juu ya nchi kavu.Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake!
7 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwangu mimi, nyinyi Waisraeli,hamna tofauti yoyote na watu wa Kushi!Niliwatoa Wafilisti kutoka Krete,na Waashuru kutoka Kiri,kama nilivyowatoa nyinyi kutoka Misri.
8 Mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nautazama ufalme wenye dhambi,na nitauangamiza kabisa kutoka duniani.Lakini sitawaangamiza wazawa wote wa Yakobo.
9 “Tazama, nitatoa amri,na kuwapepeta Waisraeli kati ya mataifakama mtu achekechavyo nafakaniwakamate wote wasiofaa.
10 Wenye dhambi miongoni mwa watu wangu,watafia vitani kwa upanga;hao ndio wasemao:‘Maafa hayatatukumba wala kutupata!’
11 “Siku yaja nitakapoisimika nyumba ya Daudi iliyoanguka;nitazitengeneza kuta zake,na kusimika upya magofu yake.Nitaijenga upya kama ilivyokuwa hapo zamani.
12 Nao Waisraeli watamiliki mabaki ya Edomuna mataifa yote yaliyokuwa yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema,na nitafanya hivyo.