8 Mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nautazama ufalme wenye dhambi,na nitauangamiza kabisa kutoka duniani.Lakini sitawaangamiza wazawa wote wa Yakobo.
9 “Tazama, nitatoa amri,na kuwapepeta Waisraeli kati ya mataifakama mtu achekechavyo nafakaniwakamate wote wasiofaa.
10 Wenye dhambi miongoni mwa watu wangu,watafia vitani kwa upanga;hao ndio wasemao:‘Maafa hayatatukumba wala kutupata!’
11 “Siku yaja nitakapoisimika nyumba ya Daudi iliyoanguka;nitazitengeneza kuta zake,na kusimika upya magofu yake.Nitaijenga upya kama ilivyokuwa hapo zamani.
12 Nao Waisraeli watamiliki mabaki ya Edomuna mataifa yote yaliyokuwa yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema,na nitafanya hivyo.
13 “Wakati waja kwa hakika,ambapo mara baada ya kulimamavuno yatakuwa tayari kuvunwa;mara baada ya kupanda mizabibuutafuata wakati wa kuvuna zabibu.Milima itabubujika divai mpya,navyo vilima vitatiririka divai.
14 Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli.Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo;watapanda mizabibu na kunywa divai yake;watalima mashamba na kula mazao yake.