1 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2 “Wewe mtu! Je, mti wa mzabibu ni bora kuliko miti mingine msituni?
3 Je, mti wake wafaa kutengenezea kitu chochote? Je, watu huweza kutengeneza kigingi kutoka mti huo ili waweze kutundikia vitu?
4 Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote?