26 Watakuvua mavazi yako na kukunyanganya johari zako nzuri.
27 Nitaukomesha uasherati na uzinzi wako ulioufanya tangu ulipokuwa kule Misri. Hutaziangalia sanamu zozote tena wala kuifikiria tena nchi ya Misri.
28 “Naam, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitakutia mikononi mwa watu unaowachukia, watu unaowaona kuwa kinyaa.
29 Na, kwa vile wanakuchukia, watakunyanganya matunda yote ya kazi yako na kukuacha uchi, bila nguo na kuonesha aibu ya uzinzi wako. Uzinzi wako na uasherati wako
30 ndivyo vilivyokuletea hali hiyo. Wewe ulizini na mataifa, ukajitia najisi kwa miungu yao.
31 Kwa kuwa ulifuata nyayo za dada yako, basi, mimi nitakupa kikombe kilekile cha adhabu ukinywe.
32 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Utakunywa toka kikombe cha dada yako;kikombe kikubwa na cha kina kirefu.Watu watakucheka na kukudharau;na kikombe chenyewe kimejaa.