29 Na, kwa vile wanakuchukia, watakunyanganya matunda yote ya kazi yako na kukuacha uchi, bila nguo na kuonesha aibu ya uzinzi wako. Uzinzi wako na uasherati wako
30 ndivyo vilivyokuletea hali hiyo. Wewe ulizini na mataifa, ukajitia najisi kwa miungu yao.
31 Kwa kuwa ulifuata nyayo za dada yako, basi, mimi nitakupa kikombe kilekile cha adhabu ukinywe.
32 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Utakunywa toka kikombe cha dada yako;kikombe kikubwa na cha kina kirefu.Watu watakucheka na kukudharau;na kikombe chenyewe kimejaa.
33 Kitakulewesha na kukuhuzunisha sana.Kikombe cha dada yako Samaria,ni kikombe cha hofu na maangamizi.
34 Utakinywa na kukimaliza kabisa;utakipasua vipandevipande kwa meno,na kurarua navyo matiti yako.Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
35 “Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa kuwa umenisahau na kunipa kisogo, basi, utawajibika kwa uasherati na uzinzi wako.”