1 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2 “Wewe mtu! Mwambie mfalme wa Tiro kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Wewe una kiburi cha moyo,na umesema kwamba wewe ni mungu,kwamba umekalia kiti cha enzi cha miungu,umekaa mbali huko baharini.Lakini, wewe ni binadamu tu wala si Mungu,ingawa wajiona kuwa una hekima kama Mungu.
3 Haya! Wewe wajiona mwenye hekima kuliko Danieli,wadhani hakuna siri yoyote usiyoijua.
4 Kwa hekima na akili yakoumejipatia utajiri,umejikusanyia dhahabu na fedhaukaziweka katika hazina zako.