11 Tena neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
12 “Wewe mtu! Imba wimbo wa maombolezo juu ya mfalme wa Tiro. Mwambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Wewe mfalme wa Tiro ulikuwa upeo wa ukamilifu;ulijaa hekima na uzuri kamili.
13 Ulikaa Edeni, bustani ya Mungu.Ulipambwa kwa kila namna ya johari,akiki, topazi, yaspi, zabarajadi, berili,sardoniki, johari ya rangi ya samawati, almasi na zumaridi.Ulikuwa na mapambo ya dhahabu.Yote uliwekewa tayari siku ulipoumbwa.
14 Nilimteua malaika kukulinda,uliishi katika mlima wangu mtakatifuna kutembea juu ya vito vinavyometameta.
15 Uliishi maisha yasiyo na lawama,tangu siku ile ulipoumbwa,hadi ulipoanza kufanya uovu.
16 Ufanisi wa biashara yakoulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi.Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa,mbali na mlima wangu mtakatifu.Na yule malaika aliyekulindaakakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.
17 Ulikuwa na kiburikwa sababu ya uzuri wako.Uliharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.Nilikubwaga chini udongoni,nikakufanya kuwa kioja kwa wafalme.