17 Ulikuwa na kiburikwa sababu ya uzuri wako.Uliharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.Nilikubwaga chini udongoni,nikakufanya kuwa kioja kwa wafalme.
18 Kwa wingi wa uhalifu wakona udanganyifu katika biashara yakoulipachafua mahali pako pa ibada;kwa hiyo nilizusha moto kwako, nao ukakuteketeza,nami nikakufanya majivu juu ya nchi,mbele ya wote waliokutazama.
19 Wote wanaokufahamu kati ya mataifawameshikwa na mshangao juu yako.Umeufikia mwisho wa kutisha,na hutakuwapo tena milele.”
20 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
21 “Wewe mtu! Ugeukie mji wa Sidoni,
22 utoe unabii juu yake kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mimi nitapambana nawe Sidoni,na kuudhihirisha utukufu wangu kati yako.Nitakapotekeleza hukumu zangu juu yakona kukudhihirishia utakatifu wangu,ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
23 Nitakupelekea maradhi mabayana umwagaji damu utafanyika katika barabara zako.Utashambuliwa kwa upanga toka pande zotena watu wako watakaouawa, watakuwa wengi.Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”