20 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
21 “Wewe mtu! Ugeukie mji wa Sidoni,
22 utoe unabii juu yake kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mimi nitapambana nawe Sidoni,na kuudhihirisha utukufu wangu kati yako.Nitakapotekeleza hukumu zangu juu yakona kukudhihirishia utakatifu wangu,ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
23 Nitakupelekea maradhi mabayana umwagaji damu utafanyika katika barabara zako.Utashambuliwa kwa upanga toka pande zotena watu wako watakaouawa, watakuwa wengi.Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
24 Mungu asema, “Mataifa jirani na Waisraeli ambayo yalikuwa yanawaudhi hayataweza tena kuwaumiza Waisraeli kama vile kwa miiba na michongoma. Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
25 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya na kuwaleta Waisraeli kutoka katika mataifa yote ambamo walitawanywa. Hivyo nitawafanya watu wa mataifa waone kuwa mimi ni mtakatifu. Watu wa Israeli wataishi katika nchi yao ambayo mimi nilimpa mtumishi wangu Yakobo.
26 Watakaa humo salama salimini; watajenga nyumba na kupanda mizabibu. Wataishi bila hofu maana mataifa jirani zao ambayo yaliwaudhi, mimi nitayaadhibu. Hapo watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.”