4 Kwa hekima na akili yakoumejipatia utajiri,umejikusanyia dhahabu na fedhaukaziweka katika hazina zako.
5 Kwa busara yako kubwa katika biasharaumejiongezea utajiri wako,ukawa na kiburi kwa mali zako!
6 Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Kwa vile unajiona mwenye hekima kama Mungu,
7 basi nitakuletea watu wageni,mataifa katili kuliko yote.Wataharibu fahari ya hekima yakona kuchafua uzuri wako.
8 Watakutumbukiza chini shimoni,nawe utakufa kifo cha kikatili kilindini mwa bahari.
9 Je, utajiona bado kuwa mungumbele ya hao watakaokuua?Mikononi mwa hao watakaokuangamiza,utatambua kuwa wewe ni mtu tu, wala si Mungu!
10 Utakufa kifo cha aibu kubwamikononi mwa watu wa mataifa.Ni mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”