8 Watakutumbukiza chini shimoni,nawe utakufa kifo cha kikatili kilindini mwa bahari.
9 Je, utajiona bado kuwa mungumbele ya hao watakaokuua?Mikononi mwa hao watakaokuangamiza,utatambua kuwa wewe ni mtu tu, wala si Mungu!
10 Utakufa kifo cha aibu kubwamikononi mwa watu wa mataifa.Ni mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
11 Tena neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
12 “Wewe mtu! Imba wimbo wa maombolezo juu ya mfalme wa Tiro. Mwambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Wewe mfalme wa Tiro ulikuwa upeo wa ukamilifu;ulijaa hekima na uzuri kamili.
13 Ulikaa Edeni, bustani ya Mungu.Ulipambwa kwa kila namna ya johari,akiki, topazi, yaspi, zabarajadi, berili,sardoniki, johari ya rangi ya samawati, almasi na zumaridi.Ulikuwa na mapambo ya dhahabu.Yote uliwekewa tayari siku ulipoumbwa.
14 Nilimteua malaika kukulinda,uliishi katika mlima wangu mtakatifuna kutembea juu ya vito vinavyometameta.