12 Wewe utajua ya kwamba mimi mwenyewe Mwenyezi-Mungu nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa dhidi ya milima ya Israeli, ukisema: ‘Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Tumepewa sisi tuinyakue!’
13 Nimesikia jinsi unavyojigamba na kusema maneno mengi dhidi yangu.
14 Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitakapokufanya wewe Edomu kuwa jangwa, dunia yote itafurahi
15 kama wewe ulivyofanya wakati nchi ya Waisraeli ilipoharibiwa. Utakuwa jangwa, ewe mlima Seiri, pamoja na nchi yote ya Edomu. Ndipo watu watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”