3 Uambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi napambana nawe, ee mlima Seiri. Ninanyosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya uwe jangwa na ukiwa.
4 Ninaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa jangwa. Ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
5 Ulikuwa adui wa daima wa Israeli, ukasababisha watu wake wauawe kwa upanga, wakati wa msiba wao, wakati wa adhabu yao ya mwisho.
6 Kwa hiyo, kama niishivyo, nasema mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, naapa kwamba kifo kinakungoja na hutaweza kukikwepa. Kwa kuwa unayo hatia ya mauaji, basi mauaji nayo yatakuandama.
7 Nitaufanya mlima Seiri kuwa ukiwa na jangwa na yeyote apitaye huko nitamwangamiza.
8 Nitajaza milima yako watu waliouawa; na katika vilima vyako na mabonde yako na magenge yako yote watakuwako waliouawa kwa upanga.
9 Nitakufanya kuwa jangwa milele, na miji yako haitakaliwa tena. Ndipo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.