12 Mtawala anapotaka kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kwa hiari, iwe sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, watamfungulia lango la ukumbi wa ndani unaoelekea mashariki. Atatoa sadaka kama anavyofanya siku ya sabato, na anapotoka, lango lifungwe nyuma yake.
13 “Kila siku asubuhi mtamtolea Mwenyezi-Mungu mwanakondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, ambaye atateketezwa mzima.
14 Pia kila siku, sadaka ya kilo mbili za unga itatolewa asubuhi pamoja na lita moja ya mafuta ya zeituni yakichanganywa na unga. Ni lazima kufuata sheria za sadaka hii kwa Mwenyezi-Mungu milele.
15 Mwanakondoo, unga na mafuta ni lazima vitolewe kila siku asubuhi kwa Mwenyezi-Mungu milele.
16 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ikiwa mtawala anampa mmojawapo wa wanawe zawadi ya ardhi, zawadi hiyo itakuwa mali ya huyo kijana milele kama sehemu ya jamaa yake.
17 Lakini ikiwa atampa mmoja wa watumishi wake sehemu yoyote ya ardhi yake, zawadi hiyo itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuachwa huru. Ndipo itakapomrudia mtawala. Ni yeye tu na watoto wake wa kiume wanaoweza kuimiliki daima.
18 Mtawala kamwe asipore mali ya watu. Ardhi yoyote anayowapa watoto wake wa kiume ni lazima itokane na eneo lake mwenyewe. Hivyo hatawadhulumu watu wangu kwa kuwanyanganya ardhi yao.”