2 Kisha akanipeleka nje kwa njia ya lango la kaskazini. Akanizungusha kwa njia ya nje mpaka lango la nje, upande wa mashariki; na maji yalikuwa yanatoka upande wa kusini.
3 Yule mtu, kwa ufito wake wa kupimia, akapima mita 500 kwenda chini upande wa mashariki, akanipitisha kwenye maji. Maji yalifika kwenye nyayo tu.
4 Kisha akapima tena mita 500, akaniongoza kuvuka maji. Maji yakafika mpaka magoti yangu. Akapima tena mita nyingine 500, naye akaniongoza kuvuka maji. Maji yakafika mpaka kiunoni mwangu.
5 Akapima mita 500 nyingine, na mto ukawa na kilindi kirefu hata sikuweza kuuvuka tena. Haikuwezekana kuuvuka ila kwa kuogelea.
6 Yule mtu akaniambia, “Wewe mtu! Zingatia mambo hayo yote kwa makini.”Kisha, akanirudisha mpaka ukingo wa mto.
7 Nilipofika huko niliona miti mingi sana kwenye kingo za mto.
8 Akaniambia, “Maji haya yanatiririka kupitia nchini hadi Araba; na yakifika huko yatayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji mazuri.