2 “Tuma watu waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani ambayo ninawapa wana wa Israeli. Utatuma mtu mmoja kutoka katika kila kabila, na mtu huyo lazima awe kiongozi katika kabila lake.”
3 Basi, kwa mujibu wa agizo la Mwenyezi-Mungu, Mose akatuma watu kutoka jangwa la Parani. Watu wote waliotumwa walikuwa viongozi wa makabila mbalimbali ya wana wa Israeli.
4 Ifuatayo ndiyo orodha ya majina ya watu hao:Kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri.
5 Kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori.
6 Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
7 Kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu.
8 Kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni.