1 Baada ya yale maradhi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni,
2 “Hesabuni jumuiya yote ya Waisraeli, kila mtu kufuatana na jamaa yake. Wahesabuni watu wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi wanaofaa kwenda jeshini.”
3 Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia,
4 “Hesabuni watu kuanzia na wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.” Idadi ya Waisraeli waliotoka Misri ni hii:
5 Kwanza ni kabila la Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Henoki, Palu,
6 Hesroni na Karmi.
7 Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730.
8 Wazawa wa Palu walikuwa Eliabu,
9 na wanawe Nemueli, Dathani na Abiramu. (Hawa wawili: Dathani na Abiramu, ndio waliokuwa wamechaguliwa miongoni mwa jumuiya, lakini wakampinga Mose na Aroni, na kujiunga na wafuasi wa Kora wakati walipomwasi Mwenyezi-Mungu.
10 Wakati huo ardhi ilifunguka ikawameza, wakafa pamoja na Kora na wafuasi wake moto ulipoangamiza watu 250; wakawa onyo kwa watu.
11 Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.)
12 Kabila la Simeoni. Nemueli, Yamini, Yakini,
13 Zera na Shauli.
14 Hizo ndizo koo za kabila la Simeoni, jumla yao wanaume 22,000.
15 Kabila la Gadi lilikuwa na jamaa za Sefoni, Hagi, Shuni,
16 Ozni, Eri,
17 Arodi na Areli.
18 Hizo ndizo koo za kabila la Gadi, jumla wanaume 40,500.
19 Kabila la Yuda lilikuwa na wanawe wa Yuda Eri na Onani. Hawa walifia nchini Kanaani.
20 Kabila la Yuda lilikuwa na jamaa za Shela, Peresi, na Zera.
21 Kutoka kwa Peresi, familia ya Hesroni na Hamuli.
22 Hizo ndizo koo za Yuda, jumla wanaume 76,500.
23 Kabila la Isakari lilikuwa na jamaa za Tola, Puva,
24 Yashubu na wa Shimroni.
25 Hizo ndizo koo za Isakari, jumla wanaume 64,300.
26 Kabila la Zebuluni lilikuwa na jamaa za Seredi, wa Eloni na wa Yaleeli.
27 Hizo ndizo koo za Zebuluni, jumla wanaume 60,500.
28 Kabila la Yosefu baba yao Manase na Efraimu.
29 Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi.
30 Yezeri, Heleki,
31 Asrieli, Shekemu,
32 Shemida na Heferi.
33 Selofehadi, mwana wa Heferi hakupata watoto wa kiume bali wa kike tu, nao ni Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirza.
34 Hizo ndizo koo za Manase, jumla wanaume 52,700.
35 Kabila la Efraimu lilikuwa na jamaa za Shuthela, Bekeri na Tahani.
36 Ukoo wa Erani ulikuwa na jamaa ya Shuthela.
37 Hizo ndizo koo za Efraimu, jumla wanaume 32,500. Zote hizo zilitokana na Yosefu.
38 Kabila la Benyamini lilikuwa na jamaa za Bela, Ashbeli, Ahiramu,
39 Shufamu na Hufamu.
40 Koo za Ardi na Naamani, zilitokana na Bela.
41 Hizo ndizo koo za Benyamini, jumla wanaume 45,600.
42 Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu;
43 ukoo ulikuwa na wanaume 64,400.
44 Kabila la Asheri lilikuwa na jamaa za Imna, Ishvi na Beria.
45 Koo za Heberi na Malkieli zilitokana na Beria.
46 Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.
47 Hizo ndizo koo za kabila la Asheri, jumla wanaume 53,400.
48 Kabila la Naftali lilikuwa na jamaa za Yaseeli, Guni,
49 Yeseri na Shilemu.
50 Hizi ndizo koo za kabila la Naftali, jumla wanaume 45,400.
51 Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730.
52 Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,
53 “Makabila haya yatagawiwa nchi iwe urithi wao, kulingana na idadi ya majina yao.
54 Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake.
55 Hata hivyo ugawaji wa nchi utafanywa kwa kura. Kila kabila litarithi kulingana na majina ya ukoo wao.
56 Urithi wa kila kabila utagawanywa kwa kura, kila kabila litapata kulingana na ukubwa au udogo wake.”
57 Hizi ndizo koo za Walawi zilizoorodheshwa na jamaa zao: Gershoni, Kohathi na Merari,
58 Pamoja na jamaa za Libni, Hebroni, Mahli, Mushi na Kora. Kohathi alikuwa baba yake Amramu.
59 Mkewe Amramu aliitwa Yokebedi binti yake Lawi, aliyezaliwa Misri. Huyu alimzalia Amramu watoto wawili wa kiume, Aroni na Mose, na binti mmoja, Miriamu.
60 Aroni alikuwa na watoto wa kiume wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
61 Nadabu na Abihu walikufa walipomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya moto usiofaa.
62 Idadi ya Walawi wanaume wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ilikuwa 23,000. Hawa hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu wao hawakupewa urithi wowote miongoni mwao.
63 Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko.
64 Miongoni mwao hakuwamo hata mtu mmoja aliyesalia kati ya wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni ambao walifanya sensa ya kwanza jangwani Sinai.
65 Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema kwamba wote watafia jangwani, na kweli hakuna hata mmoja wao aliyebaki hai, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.