1 Mwenyezi-Mungu aliwapa Mose na Aroni, maagizo yafuatayo:
2 “Waisraeli watapiga kambi zao, kila mmoja akikaa mahali penye bendera yake, penye alama za ukoo wake. Watapiga kambi zao kulizunguka hema la mkutano.
3 “Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua watakuwa kikundi cha watu walio chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu,
4 kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 74600.
5 Wale watakaofuata kupiga kambi baada ya watu wa Yuda watakuwa kabila la Isakari, kiongozi wao akiwa Nethaneli mwana wa Suari,
6 kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 54,400.
7 Kisha kabila la Zebuluni, kiongozi wao akiwa Eliabu mwana wa Heloni,