7 Kisha kabila la Zebuluni, kiongozi wao akiwa Eliabu mwana wa Heloni,
8 kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 57,400.
9 Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
10 “Kwa upande wa kusini, wale walio chini ya bendera ya kundi la Reubeni kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elisuri mwana wa Shedeuri,
11 kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 46,500.
12 Kisha wale watakaopiga kambi kando ya watu wa Reubeni watakuwa ni watu wa kabila la Simeoni, kiongozi wao akiwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai,
13 kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 59,300.