18 Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za vinywaji pamoja na wale fahali, kondoo na wanakondoo, kulingana na idadi yao.
19 Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya sadaka ya kuteketezwa ya kawaida pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
20 “Siku ya tatu mtatoa: Fahali kumi na mmoja, kondoo wawili, wanakondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
21 Mtawatolea pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji kama ilivyotakiwa kulingana na idadi yao.
22 Vilevile mtatoa beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
23 “Siku ya nne mtatoa: Fahali kumi, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne, wasio na dosari.
24 Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali na kondoo na wanakondoo kulingana na idadi yao, kama inavyotakiwa.