39 “Haya ndiyo maagizo kuhusu sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na sadaka za amani mtakazomtolea Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu zenu zilizopangwa. Licha ya hizi zote, zipo pia sadaka za kuteketezwa, za nafaka na za kinywaji, ambazo mnamtolea Mwenyezi-Mungu kutimiza nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari.”