10 Utawateua Aroni na wanawe ili waweze kutekeleza huduma zao za ukuhani; lakini kama mtu yeyote mwingine atakaribia, atauawa.”
11 Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Mose,
12 “Angalia, sasa nimewateua Walawi miongoni mwa Waisraeli wote, badala ya kila mzaliwa wa kwanza wa kiume kifunguamimba katika kila familia ya Israeli. Walawi ni wangu,
13 kwani kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri nilijiwekea wakfu kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli; kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu hata wa mnyama; wao watakuwa wangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
14 Baadaye Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose katika jangwa la Sinai,
15 “Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.”
16 Basi, Mose akawahesabu kufuatana na neno la Mwenyezi-Mungu, kama alivyomwamuru.