13 kwani kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri nilijiwekea wakfu kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli; kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu hata wa mnyama; wao watakuwa wangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
14 Baadaye Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose katika jangwa la Sinai,
15 “Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.”
16 Basi, Mose akawahesabu kufuatana na neno la Mwenyezi-Mungu, kama alivyomwamuru.
17 Wafuatao ndio waliokuwa wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
18 Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni kwa kufuata familia zao: Libni na Shimei.
19 Wana wa Kohathi kwa kufuata familia zao: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.