44 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,
45 “Sasa, watenge Walawi wote kuwa wangu badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli. Kadhalika, watenge ng'ombe wa Walawi wote badala ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe wa Waisraeli. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
46 Kwa ajili ya fidia ya wazaliwa wa kwanza wa kiume wa watu wa Israeli 273, wanaozidi idadi ya wanaume Walawi,
47 utapokea kwa kila mwanamume fedha shekeli tano, kulingana na kipimo cha mahali patakatifu, ambayo ni sawa na gera ishirini,
48 na fedha hizo kwa ajili ya fidia ya hao waliozidi idadi yao utampa Aroni na wanawe.”
49 Mose akatii, akachukua fedha hizo za fidia ya hao waliozidi idadi ya waliofidiwa na Walawi;
50 alipokea kutoka wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli fedha kiasi cha shekeli 1,365, kulingana na kipimo cha mahali patakatifu,