1 Mwenyezi-Mungu aliongea na Mose, akamwambia,
2 “Walipize kisasi Wamidiani mambo waliyowatenda Waisraeli; kisha wewe utafariki.”
3 Basi Mose akazungumza na watu akawaambia, “Watayarisheni watu kwa vita waende kuwashambulia Wamidiani kumlipizia Mwenyezi-Mungu kisasi.
4 Kutoka kila kabila la Israeli, mtapeleka watu 1.000 vitani.”