32 Nyara walizoteka wanajeshi zilikuwa: Kondoo 675,000,
33 ng'ombe 72,000,
34 punda 61,000,
35 na wasichana ambao hawakuwa wamelala na mwanamume 32,000.
36 Nusu yake, sehemu ambayo iligawiwa wanajeshi waliokwenda vitani, ilikuwa kondoo 337,500,
37 katika hao 675 walitolewa kwa Mwenyezi-Mungu.
38 Ngombe wa wanajeshi walikuwa 36,000, na katika hao 72 walitolewa zaka kwa Mwenyezi-Mungu.