17 “Kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni ndio watakaowagawia watu nchi kuwa mali yao.
18 Utachukua pia kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia katika ugawaji wa nchi.
19 Haya ndiyo majina yao:Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
20 Kabila la Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21 Kabila la Benyamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
22 Kabila la Dani, Buki mwana wa Yogli.
23 Kabila la Manase mwanawe Yosefu, Hanieli mwana wa Efodi.