1 Watu wa Efraimu wananirundikia uongo,na Waisraeli udanganyifu.Watu wa Yuda, wananiasi mimi Mungu Mtakatifu.
2 “Watu wa Efraimu wanachunga upepokutwa nzima wanafukuza upepo wa mashariki.Wanazidisha uongo na ukatili,wanafanya mkataba na Ashuruna kupeleka mafuta Misri.”
3 Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya Yuda;atawaadhibu wazawa wa Yakobo kadiri ya makosa yao,na kuwalipa kadiri ya matendo yao.
4 Yakobo akiwa bado tumboni mwa mama yake,alimshika kisigino kaka yake.Na alipokuwa mtu mzimaalishindana na Mungu.
5 Alipambana na malaika, akamshinda;alilia machozi na kuomba ahurumiwe.Huko Betheli, alikutana na Mungu,huko Mungu aliongea naye.